Mo Salah adokeza huenda akastaafu kwenye kandanda baada ya kukatishwa tamaa kushiriki Kombe la Dunia

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 alianza soka  akiwa na timu ya taifa ya Misri mwaka 2011.

0
Mohamed Salah wa timu ya Misri

Mohamed Salah amezua shaka kuhusu mustakabali wake na timu ya taifa ya Misri kufuatia kushindwa kufuzu kwa Kombe la Dunia.

Katika maoni kwa timu yake kwenye video iliyochapishwa na wizara ya vijana na michezo ya Misri, beki huyo wa Liverpool alisema jinsi anavyojivunia timu hiyo.

Pharoahs walishindwa na Senegal kwa mikwaju ya penalti siku ya Jumanne.

Video hiyo inamuonyesha Salah akiwahutubia wachezaji wenzake kwenye vyumba vya kubadilishia nguo baada ya kushindwa kwao, akisema: “Niliwaambia wachezaji jana (kabla ya mechi) kwamba ninajivunia kucheza nao, na kwamba ni miongoni mwa wachezaji bora ambao nimecheza nao.”

“Hakuna mengi ya kusema, lakini imekuwa heshima kuu kucheza nanyi, iwe niko hapa au la.”

Matamshi ya Salah yanatafsiriwa kama ishara kwamba anaweza kuwa tayari kustaafu soka ya kimataifa.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 alianza soka  akiwa na timu ya taifa ya Misri mwaka 2011.

Moja ya mafanikio yake ya taji ni kufunga bao la dakika za mwisho katika mechi ya kufuzu kwa Kombe la Dunia 2017 dhidi ya Congo, na kuipeleka Misri kwenye Kombe la Dunia la 2018 nchini Urusi.

Siku ya Jumanne, Salah alikosa kufunga penalti dhidi ya Senegal.

Ni mara ya pili ndani ya miezi miwili kwa Pharoahs hao kushindwa kutamba mbele ya Senegal baada ya Simba wa Teranga kuwafunga kwenye fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika mwezi Februari, katika mechi ambayo pia ilimalizika kwa mikwaju ya penalti.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted