#Kenya: Rais mstaafu Mwai Kibaki aaga dunia

Rais wa zamani wa Kenya Mwai Kibaki, ambaye aliongoza Kenya kwa zaidi ya muongo mmoja amefariki dunia,

0
Emilio Mwai Kibaki, Raia wa tatu wa Kenya

Rais wa zamani wa Kenya Mwai Kibaki, ambaye aliongoza Kenya kwa zaidi ya muongo mmoja amefariki dunia, Rais wa sasa Uhuru Kenyatta ametangaza Ijumaa.

Alikuwa na umri wa miaka 90.

Alihudumu kama Makamu wa nne wa Rais wa Kenya kwa miaka kumi kutoka 1978 hadi 1988 chini ya Rais Daniel arap Moi.

Pia alishikilia wadhfa wa waziri katika serikali za Kenyatta na Moi, na pia kama waziri wa Fedha (1969-1981) chini ya Kenyatta, na Waziri wa Mambo ya Ndani (1982-1988) na Waziri wa Afya (1988-1991) chini ya Rais wa pili wa Kenya Daniel Arap Moi.

Kibaki aliwahi kuwa Mbunge wa upinzani kuanzia 1992 hadi 2002. Aligombea urais bila mafanikio mwaka 1992 na 1997. Aliwahi kuwa Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kuanzia 1998 hadi 2002.

“Ni siku ya huzuni kwetu kama nchi. Tumempoteza kiongozi wwakutegemewa,” Kenyatta alisema katika hotuba yake kwenye televisheni ya taifa.

Kenyatta ametangaza kipindi cha maombolezo ya kitaifa hadi  Kibaki atakapozikwa, na bendera zote kupeperushwa nusu mlingoti.

Kibaki alihudumu kama rais wa tatu wa Kenya, kuanzia 2002 hadi 2013.

 “Kama kiongozi mkuu katika historia ya baada ya uhuru wa Kenya… Kibaki alipata heshima na mapenzi ya watu wa taifa hili,” Kenyatta alisema.

“Rais Kibaki atakumbukwa milele kama muungwana katika siasa za Kenya.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted