Uhuru, Ruto wakaa mbali mbali katika mkutano wa maombi ya kitaifa

Wakati wa hafla hiyo iliyofanyika katika Hoteli ya Safari Park jijini Nairobi, Uhuru na Ruto walikaa kwa utulivu kila mmoja akishiriki kwenye meza yake tofauti.

0
Rais Uhuru Kenyatta katika hoteli ya Safari Park jijini Nairobi kwenye maombi ya Kitaifa

Mvutano kati ya Rais Uhuru Kenyatta na Naibu Rais William Ruto uliibuka tena Alhamisi kwenye maombi ya kitaifa baada ya viongozi hao wawili ambao wamekuwa wakishiriki meza moja walikaa meza mbali mbali.

Wakati wa hafla hiyo iliyofanyika katika Hoteli ya Safari Park jijini Nairobi, Uhuru na Ruto walikaa kwa utulivu kila mmoja akishiriki kwenye meza yake tofauti.

Rais Kenyatta alishiriki meza yake na Jaji Mkuu Martha Koome na Mwanasheria Mkuu Kihara Kariuki.

Ruto alishiriki meza yake na Spika wa Bunge la Kitaifa Justin Muturi na mwenzake wa Seneti Ken Lusaka, washirika wake wote katika Muungano wa Kenya Kwanza.

Kaulimbiu katika maombi yakitaifa ya mwaka huu ni ‘mpito’ ambayo inakuja miezi miwili tu kabla ya nchi kwenda kwa Uchaguzi Mkuu.

Na ingawa mkutano huo wa maombi unakusudiwa kuhubiri umoja wa kitaifa katika wakati mgumu wakati nchi inaelekea kwenye uchaguzi, haikuwa hivyo.

Rais Kenyatta na naibu wake wamegeuka kuwa maadui wakubwa ambao mara nyingi wanajihusisha na majibizano makali ya umma huku siasa za urithi zikipamba moto.

Kenyatta ametangaza hadharani kwamba ‘hatamruhusu’ Ruto kumrithi.

Makubaliano ya Machi 9, 2018 kati ya Rais Kenyatta na mpinzani wake wa zamani Odinga yalivuruga uhusiano mzuri uliokuweko kati ya Naibu Rais Ruto na Rais Uhuru Kenyatta.

Rais Kenyatta alisema mara nyingi kwamba Ruto atamrithi pindi atakapoondoka madarakani 2022 lakini baada ya kura za 2017, Rais alipitisha msimamo tofauti akisema chaguo lake la mrithi ‘litashtua nchi.’

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted