Chama Cha UDA Chafanya Mabadiliko Katika Uongozi Wake

Gavana wa Embu Cecily Mbarire ameteuliwa kama mwenyekiti wa chama cha United Democratic Alliance (UDA) Chake rais William Ruto.

0

Gavana wa Embu Cecily Mbarire ameteuliwa kama mwenyekiti wa chama cha United Democratic Alliance (UDA) Chake rais William Ruto.


Katika mabadiliko yaliyofanywa Jumatatu,Gavana Mbarire anachukua nafasi ya aliyekuwa seneta wa kaunti ya Machakos Johnson Muthama ambaye alijiuzulu.


Muthama ameteuliwa kama mwanachama wa huduma kwa bunge (PSC ) Kulingana na ripoti iliyowasilishwa katika bunge la kitaifa na lile la seneti.


Muthama anatarajiwa kuchukua nafasi ya mbunge wa Ainabkoi Samuel Chepkong’a ambaye alijiuzulu kutoka nafasi hiyo ili kutetea kiti cha ubunge.


Katika mabadiliko mengine,aliyekuwa seneta wa Kakamega Cleophas Malala ameteuliwa kama katibu mkuu mpya wa chama cha UDA.


Malala anaziba nafasi iliyowachwa wazi na Veronica Maina ambaye aliyeteuliwa katika bunge la Seneti.
Mabadiliko haya yanafuatia kikao cha kamati kuu ya kitaifa ya kilichoandaliwa Jumatatu.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted