Mbappe kuwa nahodha mpya wa Ufaransa

Mbappe, 24, alikubali jukumu hilo baada ya mazungumzo na kocha Didier Deschamps

0

Kylian Mbappe atachukua nafasi ya nahodha wa Ufaransa baada ya Hugo Lloris kujiuzulu kufuatia kushindwa kwa fainali ya Kombe la Dunia dhidi ya Argentina, chanzo cha karibu na timu hiyo kimesema.

Mbappe, 24, alikubali jukumu hilo baada ya mazungumzo na kocha Didier Deschamps.

Mchezo wake wa kwanza kama nahodha utakuwa wa Ijumaa wa kufuzu kwa Euro 2024 dhidi ya Uholanzi Uwanja wa Stade de France, mechi ya kwanza ya Les Bleus tangu kukatishwa tamaa kwa fainali ya Kombe la Dunia huko Doha mnamo Desemba 18.

Kipa wa Tottenham Lloris, 36, alimaliza soka lake la kimataifa mwezi Januari, wiki chache baada ya kikosi cha Lionel Messi cha Argentina kuwashinda Wafaransa hao kwa mikwaju ya penalti kufuatia mechi ya kusisimua iliyoisha 3-3 katika muda wa ziada.

Lloris alikuwa nahodha kwa zaidi ya muongo mmoja.

Mshambulizi wa Atletico Madrid Antoine Griezmann alitangazwa kuwa makamu wa nahodha baada ya beki wa kati wa Manchester United Raphael Varane pia kutundika daruga zake kufuatia kushindwa na Argentina mwezi Desemba.

Mbappe, ambaye alifunga hat-trick kwenye fainali ya Kombe la Dunia, alikuwa akihusishwa pakubwa na nafasi ya unahodha kwa wiki kadhaa.

Michel Platini, ambaye alikuwa nahodha wa Ufaransa na kupata ushindi katika michuano ya Ulaya mwaka 1984, alisema uamuzi huo ni “wazo zuri sana”.

“Katika kumpa jukumu la unahodha, inamruhusu Kylian, inapobidi, kusonga mbele zaidi, juu zaidi, na nguvu zaidi,” Platini, mkuu wa zamani wa shirikisho la soka la Ulaya UEFA, alisema katika taarifa yake.
Mbappe aliisaidia Les Bleus kutwaa ubingwa wa Kombe la Dunia akiwa kijana mwaka 2018 na amejidhihirisha kuwa mchezaji anayeongoza kwa kiwango cha kimataifa.

Mchezaji huyo wa zamani wa Monaco mzaliwa wa Paris ni makamu wa nahodha wa PSG nyuma ya mlinzi Mbrazil Marquinhos na aliongoza timu hiyo kukosekana kwa beki huyo wakati wa kupoteza kwa Rennes Jumapili.

Mbappe amefunga mabao 19 katika mechi 24 za Ligue 1 msimu huu na kuchangia mabao saba katika mbio za PSG kutinga hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, ambapo walitolewa na Bayern Munich.

Ufaransa imepangwa pamoja na Uholanzi, Jamhuri ya Ireland, Ugiriki na Gibraltar katika kundi lao la kufuzu kwa Euro 2024, itakayofanyika Ujerumani.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted