Wanaharakati wa Afrika wahimiza vijana kuwa wastahimilivu kujenga Afrika bora

Wanaharakati hao walitakiwa kuzungumza katika mkutano huo uliopewa jina la ‘The Convention 2024,’ lakini hafla hiyo ilisitishwa dakika za mwisho siku ya Jumapili.

0
Wanaharakati Peter Obi kutoka Nigeria, Dk Arikana Chihombori-Quao kutoka Zimbabwe na Profesa P. L. O. Lumumba kutoka Kenya katika Kongamano la ‘Igniting The Voices of Africa,’ lililoandaliwa na New Africa Foundation, mjini Accra, Ghana tarehe 8 Januari 2024.

Wanaharakati wa Afrika wanaosifika, Profesa P. L. O. Lumumba kutoka Kenya, Dk Arikana Chihombori-Quao kutoka Zimbabwe, na Peter Obi kutoka Nigeria kwa pamoja wamewahimiza vijana nchini Ghana na Afrika kuendelea kuwa wastahimilivu na “kusaidia kujenga Afrika tunayoitaka.”

Wanaharakati hao walitakiwa kuzungumza katika mkutano huo uliopewa jina la ‘The Convention 2024,’ lakini hafla hiyo ilisitishwa dakika za mwisho siku ya Jumapili.

‘The Convention 2024,’ uliandaliwa na Wakfu wa New Africa Foundation unaofadhiliwa na Shirika Lisilo la Kiserikali (NGO).

Baada ya kusitishwa kwa hafla hiyo, Dk Arikana, daktari na Balozi wa zamani wa Umoja wa Afrika, aliwaambia waandishi wa habari kuwa Taasisi hiyo iliwaomba wazungumzaji wawe nchini Ghana kuhutubia vijana wa Kiafrika kuanzia na vijana nchini Ghana lakini ilikatishwa saa chache kabla kuanza kwa programu.

Profesa PLO Lumumba alisema, “tulikuja Ghana kushiriki ujumbe wa matumaini ambao Afrika inahitaji kwa wakati huu na hakuna mahali pazuri pa kuanza ujumbe huo kuliko Accra Ghana.

“Ni huko Accra ambapo Osageyefo Kwame Nkrumah karibu miaka 67 iliyopita, alizungumza na dunia na kusema ‘Uhuru wa Ghana hauna maana hadi uhusishwe na uhuru wa Bara la Afrika'”. Alisema miaka 67 baadaye, walikuwa wakikusanyika huko Accra mahali pale ambapo waanzilishi wa Ghana walisimama kutoa kauli hiyo lakini walizuiliwa kwa njia ya ajabu.

Profesa PLO Lumumba, hata hivyo, alisema, “Ujumbe utatolewa” kwani safari ya matumaini “inaendelea kwa vijana.”

Lumumba alisema Waafrika wanatoa heshima kwa Ghana kutokana na kile Nkrumah alichofanya na kukisimamia.

Kwa upande wake, mwanasiasa wa Nigeria Peter Obi alisema, “Afrika inateseka kutokana na ukosefu wa uongozi. Ni uongozi ulioshindwa kwa miaka mingi ndio umeifikisha Afrika hapa ilipo.”

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted