Heche Asimulia Matukio Ya Utekaji, Kesi Za Kisiasa Na Shambulio La Lissu
Shahidi wa upande wa utetezi katika kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu, John Heche, ameieleza Mahakama matukio mbalimbali ya mauaji, utekaji na kupotezwa kwa watu nchini, akitaja viongozi na wanachama wa vyama vya siasa waliopitia matukio hayo.