Hichilema ashinda muhula mwingine wa urais Zambia kwa asilimia 60
Ushindi wa Hichilema, mwenye umri wa miaka 64, ulitarajiwa kwa kiasi kikubwa. Alikuwa akikabiliwa na wagombea 13, akiwemo aliyekuwa waziri wa zamani wa mkoa, Brian Mundubile, ambaye alikuwa akigombea urais kwa mara ya kwanza.