Tanzania
-

Serikali yatoa sababu za kusitisha zoezi la utambuzi wa mifugo kwa kutumia hereni za kieletroniki.
Kauli hiyo imetolewa leo bungeni Dodoma na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati wa kipindi cha maswali ya papo kwa papo.
-

Bodi ya Mikopo Tanzania yaendelea kuandamwa, yadaiwa kutoa mikopo ya shilingi bilioni 1 kwa wanafunzi wasiostahili.
Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (PAC) imebaini utoaji wa mikopo inayofikia shilingi bilioni 1.76 kwa wanafunzi wasiostahili katika kipindi cha kati ya mwaka 2016 hadi mwaka 2018.
-

Mradi wa visima vya maji kupunguza adha ya upatikanaji maji Dar
Mradi huo unahusisha visima saba na tenki la kuhifadhia maji lenye ukubwa la lita 15 milioni unatekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira (Dawasa) umekamilika kipindi ambacho jiji la Dar es Salaam lina…
-

Adaiwa kumuua mwanaye kwa kipigo
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoani Mwanza, Maili Makori amesema wanawasaka wazazi wa mtoto huyo waliotoweka mara baada ya mauaji hayo.
-

Tanzania yatuma wanajeshi kuzima moto mlima Kilimanjaro
Moto huo ulianza tarehe 21 mwezi oktoba karibu na eneo la Karanga linalotumiwa sana na wanaokwea mlima huo.
-

Simbachawene: Serikali ilitumia bilioni 17 kwa waathirka wa mabomu Mbagala
Simbachawene ameyasema hayo leo bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la mbunge wa jimbo la Mbagala, Abdalah Chaurembo aliyetaka kufahamu kauli ya serikali juu ya mapunjo ya fidia kwa wananchi walioathirika na mlipuko wa mabomu…
-

Dawa ya ganzi yatajwa kuwa chanzo cha vifo kwa wanawake kutokana na uzazi nchini Tanzania
Kwa mujibu wa Naibu Waziri wa Afya nchini Tanzania, Dkt Godwin Mollel ni kwamba wanawake 263 wamepoteza maisha kutokana na uzazi katika kipindi cha mwaka 2018 hadi 2021, huku miongoni mwa sababu zikielezwa kuwa ni…
-

Bei mafuta yaendelea kupungua nchini Tanzania
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana tarehe 1 Novemba 2022 na Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Modestus Lumato, ilieleza kuwa bei hizo zitaanza kutumika leo tarehe 2 Novemba, 2022 saa 6.00 usiku, zimeshuka ikilinganishwa na bei…
-

Rais Samia aunda Kikosi Kazi cha kushughulikia Nishati Safi ya Kupikia
Rais Samia Suluhu ameshiriki katika Kongamano la Nishati safi iliyoandaliwa na Wizara ya Nishati chini ya Waziri January Makamba.
-

TANZANIA: Idadi ya watu imepanuka na kufikia milioni 16 katika muongo mmoja- Rais Samia
Jumla ya watu wote Tanzania ni 61,741,120 kati ya hao watu 59,851,357 wapo Tanzania bara na watu 1,889,773 wapo Zanzibar







