SHAHIDI AELEZA MIPANGO YA MBOWE KUMDHURU SABAYA

Shahidi wa pili katika kesi ya Uhujumu Uchumi yenye makosa ya Ugaidi ndani yake inayomkabili mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe na wenzake watatu leo ameileza mahakama jinsi ambavyo...

0

Shahidi wa pili katika kesi ya Uhujumu Uchumi yenye makosa ya Ugaidi ndani yake inayomkabili mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe na wenzake watatu leo ameileza mahakama jinsi ambavyo Mbowe alivyokua na mkakati wa kutaka kumdhuru aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai Lengai Ole.

Shahidi huyo wa pili kati ya mashahidi 24 waliopangwa kuletwa na upande wa Jamhuri Jastine Kaaya (31) mkazi wa Longido jijini Arusha anayejishughulisha na kilimo cha mboga mboga amesema kabla ya kujihusisha na shughuli hiyo amewahi kufanya kazi ya upigaji picha za mnato katika kipindi cha mwaka 2017 na alikua mara nyingi anawapiga picha viongozi mbalimbali wakiwemo wanasiasa.Akihojiwa na Wakili mwandamizi wa Serikali Abdallah Chavula alimuuliza shahidi huyo kuwa ni viongozi gani ambao amewahi kuwapiga picha.Shahidi akaeleza kuwa miongoni mwa viongozi aliowahi kuwapiga picha ni Mbunge wa Longido Steven Kiluswa, aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo, aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Arusha Mjini Gabriel Ndagalo na aliwahi kuwa mkuu wa wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya.

Wakili mwandamizi Abdallah Chavula alipomtaka Shahidi kueleza kwamba Sabaya alikutana nae vipiShahidi alieleza Mahakama kwamba alijuana na Sabaya mnamo mwaka 2017, kwenye uchaguzi mdogo wa jimbo la Longido, wakati huo Sabaya akiwa ni Diwani.Kuanzia hapo Sabaya alimuomba Jastine Kaaya (Shahidi), amsaidie kupiga picha katika kazi zake, na hakuona sababu ya yeye kukataa kutokana na kuwa ni fursa kwake.Baada ya kukubali ombi la Sabaya ikabidi ahamie nyumbani kwa Sabaya sehemu inayoitwa Kibanda Maziwa kutokana na eneo alikokuwa akiishi shahidi huyo kuwa mbali na maneno aliyopo Sabaya.Shahidi ameambia Mahakama kuwa amefany kazi na Sabaya kuanzia mwaka 2017, hadi pale Sabaya alipoteuliwa kuwa mkuu wa wilaya ya Hai Alipoulizwa na wakili wa Serikali kuwa baada ya Sabaya kuteuliwa kuwa mkuu wa wilaya ya Hai alienda kuishi wapi Shahidi ameileza mahakama kwamba alikwenda kuishi nae kwenye makazi ya mkuu wa wilaya ya Hai hadi pale alipoamua kuacha kufanya nae kazi Oktoba 10, 2018.

Shahidi amesema kwamba aliamua kuachana na kazi hiyo kwa sababu alitalia kwenda nyumbani kwake Longido kuendelea na shughuli zake za kilimo tu. Wakili Chavula alimuuliza shahidi kwamba alipokuwa Longido ni mtu gani ambaye anakumbuka alifanya naye mawasilisho mnamo 2018. Shahidi alieleza kwamba siku moja akiwa nyumbani kwake Longido alipigiwa simu kwenye namba yake ya Airtel ya 0693006700 na simu hiyo ilitoka kwa mtu aliyejitambulisha kuwa ni Freeman Mbowe ambaye namba yake ilisomeka 0784779944. Ameendelea kusema kuwa alishtuka kusikia hivyo, kwa sababu hakua anafahamiana nae kwa ukaribu.Shahidi amedai kuwa kwenye mazungumzo hayo, Mbowe alimwambia shahidi huyo kuwa ana shida ya kuonana nae kwa sababu ana jambo muhimu anataka kuzungumza nae. Alipomuuliza Mbowe kuwa yupo wapi aliwambia kuwa yupo Arusha.

Shahidi akasema kwamba alimwambia Mbowe kuwa yupo Longido hivyo kuna changamoto ya usafiri.Hata hivyo kwa mujibu wa shahidi mbele ya Mahakama hiyo hii leo amesema kwamba Mbowe alimwambia achukue gari aina ya Noah na Mbowe ndiye atakayelipa gharama za usafiri huo pindi tu atakapofika Arusha. Baada ya kuambiwa hivyo na Mbowe Shahidi ameileza mahakama kwamba aliwambia hawezi kwenda kwa sababu ya hofu. Alipoulizwa na Wakili kwamba hofu ilikua ya nini, shahidi alieleza kwamba kwanza Mbowe ni kiongozi mkubwa na pia hawajawahi kufahamianaBaada ya hapo kwa maelezo ya shahidi mahakamani amesema kuwa Mbowe alikuta simu na kumwambia kuwa angempigia baadae. Shahidi amesema baada ya muda kupita, Freeman Mbowe alimpigia tena simu na kumwambia kuwa yuko njiani kuelekea Longido ambapo shahidi anaishi, na alimuelekeza kuwa wakutane kwenye uwanja wa mpira uliopo katika mji wa Longido. Kaaya (Shahidi), akiwa anaendelea kutoa ushahidi wake amesema muda huo waliokutana na Mbowe kwenye uwanja huo ilikua ni usiku majira ya saa 3 na alipofika eneo la makutano alimuona Mbowe akiwa na mwanamke mmoja ambaye yeye hakumfahamu . Wakili Chavula alipomuuliza Shahidi kuwa dhumuni la Mbowe kukutana nae lilikua lipi?

Shahidi amesema Mbowe alimwambia kuwa anataka taarifa za na shughuli anazofanya Sabaya na watu wake aliokuwa nao wilaya ya Hai. Kaaya(Shahidi) alimwambia Mbowe kuwa haitawekana kwa sababu kwa kipindi hicho hakua anafanya kazi na Sabaya.Baada ya hapo amesema Mbowe alimwambia kwamba yeye ni kiongozi wa chama kikuu cha upinzani kwenye nchi hii, hivyo atafanya namna yoyote ile ili shahidi huyo arudi tena kwa Sabaya kwenda kufanya kaziHata hivyo alimwambia Mbowe kuwa haitawezekana kwa sababu ameamua kufanya kazi binafsi.Alivyomaliza kutoa majibu hayo Shahidi ameiambia Mahakama kuwa Mbowe alimpatia shilingi laki 3 kama pesa ya usumbufu na kisha Mbowe akaondoka eneo hiloWakati Mbowe anaondoka Shahidi amesema kwamba alimpigia simu Sabaya ili ampe taarifa lakini haikupokelewa, hivyo aliamua kumpigia Mbunge wa Longido Dk. Steven Kiduswa na kumueleza.

Tangu wakati huo mwaka 2018 hakuwahi kuwasiliana tena na Mbowe hadi ilipofika mwanzoni mwa mwaka 2020, ndipo alipoweza kuwasiliana nae kwa njia ya Whatsup, ambapo Mbowe alimwambia Kaaya (Shahidi) kuwa anataka waonane akimuelekeza kuwa wakutane MoshiBaada ya kukubaliana nae walikutana na Mbowe eneo la Machame Road ambapo aliingia kwenye gari nyeusi aina ya V8 yenye bendera ya bunge. Mara baada ya hapo Shahidi huyo amesema walielekea katika hoteli ya Aishi ambapo hapo alikua na kikao naye na kubwa Mbowe alikua anataka majina ya wasaidizi wa Sabaya lakini alimwambia kua hana taarifa zozote kuhusu watu hao.Walipomaliza mazungumzo hayo Mbowe anadaiwa kumwambia Shahidi huyo kuwa angemtumia kiasi cha pesa ahadi ambayo kwa mujibu wa shahidi haikutekelezwa. Mwezi 7 mwaka 2020, Shahidi ameeleza kuwa Mbowe alimpigia tena simu kwa njia ya Whatsup akimueleza kuwa Wakutane Moshi majira ya jioni wakati huo Mbowe alikua njiani akitokea Dar es Salaam. Siku hiyo aliweza kuonana na Mbowe, ambapo walifanya kikao cha watu watatu, ambapo alikua Freeman Mbowe, mlinzi wa Mbowe Halfan Bwire ambaye kwenye kesi hii ni mshtakiwa namba moja na yeye mwenyewe.

Katika kikao hicho Mbowe amedaiwa kumwambia tena shahidi huyo amtajie majina ya wasaidizi wa Sabaya, ambapo safari hii aliamua kumtajia. Alipomaliza kutaja majina hayo shahidi amesema alimsikia Bwire akisema“Huyu Sabaya ni mtu mdogo sana nitamchezesha”Kwa mujibu wa shahidi Mbowe alimtumia shahidi huyo pesa kiasi cha shilingi laki mbili kwa njia ya simu. Alipotoka hapo hakuweza kuwasiliana tena na Mbowe kwa sababu tarehe 25 Agosti 2020 Jastine Kaaya amedai kuwa alikamatwa na polisi akiwa eneo la Makumila wilaya ya Arumeru jijini Arusha akiwa anaenda Benki kupeleka pesa. Alipoulizwa na Wakili ni kwamba alielezwa anakamatwa kwa kosa gani, Shahidi ameeleza kuwa alikamatwa kwa sababu ya kujihusisha na kufanya vitendo vya kigaidi. Amesema kuwa alitolewa Arusha ambako alikamatiwa na kuletwa kituo cha kati cha polisi jijini Dar es Salaam, ambapo hapo alifanyiwa mahojiano na Inspekta wa Polisi Omary Mahita na baada ya hapo alifikishwa katika mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu Dar es Salaam, na kusomewa mashtaka ya kushiriki vikao vya kutaka kufanya ugaidi, kula njama Za ugaidi na utakatishaji fedha.

Akiwa mahakamani hapo aliunganishwa na watuhumiwa wengine watatu waliokuwa gerezani ambao ni  Halfan Bwire, Mohamed Ling’wenya na Adam Kasekwa. Kabla ya kuunganishwa nao shahidi amesema hakuwahi kufahamiana na Adam Kasekwa wala Mohamed Ling’wenya isipokuwa Halfan Bwire ambaye alijuana nae alipomuona Moshi.Baada ya hapo alirudishwa kwenye gereza la ukonga ambapo huko alikutana na Khalid Athumani na Halfani BwireTarehe 26 Julai 2021 majira ya jioni shahidi amesema alimuona Freeman Mbowe akiletwa katika gereza la ukonga ambapo hapo inadaiwa alimwambia Shahidi huyo kuwa nimekuja kuwatoaTerehe 27 Julai 2021 Mbowe na Washatakiwa wengine waliojumuishwa kwenye kesi hiyo walifikishwa mahakama ya KisutuHata hivyo mahakama iliwafutia mashtaka washatakiwa watatu akiwemo Jastine Kaaya ambaye ndiye shahidi wa pili wa jamhuri katika kesi hii.Mara baada ya shahidi huyo kumaliza kuyasema hayo upande wa mawakili wa Serikali ukaupisha upande wa utetezi kumuuliza mtuhumiwa maswali ya dodoso ambapo Wakili Jeriamiah Mtobesya ndie aliyeanza kumuuliza maswali shahidi huyo.Hata hivyo utetezi hawakuweza kuendelea kumuuliza maswali shahidi baada ya upande wa Jamhuri kupinga hoja ya wakili Mtobesya alipomtaka shahidi asome kielelezo cha maelezo baada ya kuondolewa kwenye kesi ya ugaidi iliyokuwepo katika mahakama ya KisutuMbishano huo wa hoja za kisheria ukasababisha mahakama kusimama kwa muda ili mawakili wa pande zote mbili wajiridhishe kwenye vifungu vya sheria walivyotumia dhidi ya shahidi.

Baada ya muda Mahakama iliendelea kwa kuruhusu upande wa utetezi kuendelea kumuhoji shahidi huyo, ambapo wakili Jeremiya Mtobesya aliendelea kumuhoji shahidi.Mtobesya: Kuna sehemu yeyote ambayo katika nyalaka inasema ulikutana na Mlinzi aitwaye Bwire ? Shahidi: Haionyeshi.

Mtobesya: Je kupitia nyalaka zao kuna sehemu umeonyesha majina umeyataja kama ulivyoieleza mahakama.

Shahidi: Itakuwa Mwandishi ameyaacha maana nilitakiwa nitoe taarifa.

Mtobesya : Nilisikia ukisema mlinzi alisema atamchezesha ni mtoto mdogo. Wakili Mtobesya alikomea hapo kwenye kumuuliza maswali ya dodoso shahidi huyo, na akasimama wakili John Mallya akaendelea kumuhoji.

Mallya: Unafahamu Diwani analipwa kiasi gani ?

Shahidi: Sifahamu

Mallya: Kuna wakati ulisema unaishi nyumbani kwa Sabaya na mkewe, na tunafahamu hivi karibuni Mahakamani Sabaya aliomba huruma ya mahakama kwamba ana am chumba huyu mke uliyemtaja wewe ni yupi

Shahidi: Sijui, nachojua Sabaya alikuwa na mke

Mallya: Umesema uliacha kazi 2018 na katika maelezo yako umeandika 2017 je mahakama ichukue yapi

Shahidi: Chukua niliyoyasema maana yapo sahihi, aliyeandika itakuwa amekosea.

Mallya: Sabaya alikuwa anakulipa shilingi ngapi

Shahidi: Alikuwa ànanilipa Sh.Laki 3

Mallya: July 26, 2021 ulisema ulikutana na Mbowe gerezani na alikwambia amekuja kuwatoa, ni kweli  kesho yake mkatoka ?

Shahidi: Ni kweli kesho yake nilitoka.

Jaji Joachim Tiganga ameahirisha kesi hiyo hadi kesho Oktoba 28 ambapo shahidi huyo atakuja kwa ajili kumalizia kutoa ushahidi wake. Freeman Mbowe na wenzake watatu wanakabiliwa na kesi ya Uhujumu Uchumi yenye makosa ya Ugaidi ndani yake.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted