Sudan Kusini iko katika hatari ya kurejea vitani, Umoja wa Mataifa waonya

Taifa hilo jipya zaidi duniani limekumbwa na misukosuko tangu lilipopata uhuru mwaka 2011

0

Sudan Kusini iko katika hatari ya kurejea vitani, Umoja wa Mataifa ulionya Ijumaa, huku kuzuka kwa ghasia za kikabila na mapigano ya kisiasa yakitishia kutengua hata hatua ndogo iliyofikiwa katika kutekeleza mchakato wake wa kuleta amani.

Taifa hilo jipya zaidi duniani limekumbwa na misukosuko tangu lilipopata uhuru mwaka 2011, vikiwemo vita vya kikatili vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miaka mitano kati ya vikosi vinavyomtii Rais Salva Kiir na naibu wake Riek Machar vilivyosababisha vito vya takriban watu 400,000.

Makubaliano ya 2018 ambayo yalimaliza vita yameharibiwa na mabishano kati ya pande hasimu.

Masharti muhimu bado hayajatekelezwa, ikiwa imesalia chini ya mwaka mmoja kabla ya nchi hiyo kufanya uchaguzi.

“Kuna hatari ya kurejea kwenye migogoro,” Yasmin Sooka, mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Kibinadamu nchini Sudan Kusini, aliwaambia waandishi wa habari siku ya Ijumaa wakati wa ziara yake nchini humo.

Kushindwa kuunda jeshi la pamoja — sehemu muhimu ya mkataba wa amani — kumeunda mazingira ambayo ghasia bado zinaendelea, Umoja wa Mataifa ulisema.

Watu 32, wakiwemo watoto, waliuawa katika uvamizi wa kutumia silaha katika jimbo la Jonglei mwezi uliopita.

Kukosekana kwa utulivu wa kisiasa kumeongeza changamoto, huku Machar akikabiliwa na upinzani unaozidi kuongezeka ndani ya safu yake, huku makada wa ngazi za juu wakilalamikia kupoteza nafasi kwa chama cha Kiir.

Muungano kati ya viongozi hao wawili uliyumba na kukabiliwa na tishio jipya mwezi Agosti wakati mapigano yalipozuka kati ya makundi hasimu ya chama cha Machar, na kusababisha vifo vya takriban watu 32.

Machar alisema mapigano hayo yalilenga kuvuruga uundwaji wa jeshi la umoja, ambalo linasalia kuwa kigezo kikubwa kati yake na Kiir, huku pande hizo zikiwa bado hazijakubaliana kuhusu makubaliano ya kugawana madaraka katika suala hilo.

Sudan Kusini imepambana na vita, njaa na mgogoro wa kisiasa na kiuchumi tangu kusherehekea uhuru wake uliopiganiwa kwa bidii kutoka kwa Sudan mwezi Julai 2011. Huku kutoridhika kumeongezeka, baadhi ya wananchi wametoa wito wa kutokea maasi ya amani ili kuuangusha utawala wa sasa.

Lakini mamlaka imedhibiti maandamano, na kuwalazimu wanaharakati kujificha.

“Wajumbe wa mashirika ya kiraia ya Sudan Kusini waliokutana na Tume walisema wanaogopa kujadili hali ya haki za binadamu, kwa kuhofia kulipizwa kisasi na vyombo vya usalama vya serikali vilivyo na rekodi ya kukandamiza maoni ya kisiasa,” UN ilisema.

“Kukosekana kwa maendeleo katika utekelezaji wa vifungu muhimu vya (mpango wa amani)… kunachangia kuendelea kwa ukosefu wa usalama na kutokujali ambapo ukiukwaji wa haki za binadamu hutokea,UN ilisema.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted