Rais wa Urusi Vladamir Putin aamuru vikosi vya nyuklia kuwa tayari

Moscow ina hazina kubwa zaidi ya silaha za nyuklia na hifadhi kubwa ya makombora ya balestiki

0
Rais wa Urusi Vladamir Putin

Rais wa Urusi Vladimir Putin aliamuru wakuu wake wa ulinzi kuweka ‘vikosi vya kuzuia mashambulizi ya kinyuklia’  katika hali ya tahadhari Jumapili na kuzishutumu nchi za Magharibi kwa kuchukua hatua ‘zisizo za kirafiki’ dhidi ya nchi yake.

Mvutano wa kimataifa tayari unaongezeka kutokana na uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine, na agizo la Putin litasababisha wasiwasi zaidi.

Moscow ina hazina kubwa zaidi ya silaha za nyuklia na hifadhi kubwa ya makombora ya balestiki ambayo ni uti wa mgongo wa vikosi vya nchi hiyo kuzuia mashambulizi.

“Ninaamuru waziri wa ulinzi na mkuu wa wafanyikazi wakuu wa vikosi vya jeshi la Urusi kuweka vikosi vya kuzuia mashambulizi tayari.” Putin alisema.

“Unaona jinsi nchi za Magharibi si rafiki kwa nchi yetu katika nyanja ya kiuchumi — wametuwekea vikwazo visivyo halali,”aliongeza, katika hotuba kwenye televisheni.

“Maafisa wakuu wa nchi zinazoongoza NATO pia wanaruhusu kauli za kichokozi dhidi ya nchi yetu.” Waziri wa Ulinzi Sergei Shoigu alijibu,’naunga mkono.’

Rais wa Urusi siku ya Alhamisi aliamuru uvamizi wa Ukraine.

Vikosi vya ardhini vya Urusi vimeingia Ukraine kutoka kaskazini, mashariki na kusini lakini vimekumbana na upinzani mkali kutoka kwa wanajeshi wa Ukraine, ambao nguvu yake imeshangaza Moscow, kulingana na vyanzo vya Magharibi.

Mamlaka ya Ukraine imeeleza kuwa baadhi ya wanajeshi wa Urusi wamekata tamaa na wamechoka, wakidai kuwa makumi ya wanajeshi wamejisalimisha.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted