Mwanawe Rais Museveni atangaza kustaafu katika jeshi la Uganda

Ingawa Kainerugaba amekanusha mara kwa mara madai kwamba ana nia ya kumrithi babake waangalizi wanaashiria kupanda kwake haraka kupitia safu ya jeshi la Uganda kama thibitisho kwamba alikuwa...

0
Meja Jenerali Muhoozi Kainerugaba (Photo by PETER BUSOMOKE / AFP)

Muhoozi Kainerugaba, mwanawe Rais wa Uganda Yoweri Museveni, alitangaza Jumanne kwamba anastaafu kutoka jeshi, na hivyo kuzua uvumi wa uwezekano wa kuwania urais mwaka wa 2026.

Ingawa Kainerugaba amekanusha mara kwa mara madai kwamba ana nia ya kumrithi babake mwenye umri wa miaka 77 –ambaye ni mmoja wa viongozi waliohudumu muda mrefu zaidi barani Afrika — waangalizi wanaashiria kupanda kwake haraka kupitia safu ya jeshi la Uganda kama thibitisho kwamba alikuwa akiandaliwa kwa ajili ya kazi hiyo ya urais..

“Baada ya miaka 28 ya utumishi katika jeshi langu tukufu, nina furaha kutangaza kustaafu kwangu,” jenerali huyo mwenye umri wa miaka 47 alisema kwenye Twitter, bila kutoa maelezo zaidi kuhusu uamuzi wake.

“Mimi na askari wangu tumefanikiwa sana! Nina upendo na heshima tu kwa wanaume na wanawake wote wakuu ambao wanafanikisha ukuu kwa Uganda kila siku.”

Ameongoza vikosi vya nchi kavu vya Uganda na anahudumu kama mshauri wa rais katika operesheni maalum — jukumu ambalo linahusishwa na nyanja ya kisiasa.

Mtumiaji mahiri wa mitandao ya kijamii, Kainerugaba mara kwa mara huingia kwenye mizozo, mara nyingi akitweet kuhusu sera za kigeni.

Hivi majuzi zaidi, alijitenga na Umoja wa Afrika katika kutangaza kuunga mkono uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, akiandika kwenye ukurasa wa Twitter mwezi uliopita: Watu wengi (ambao si wazungu) wanaunga mkono msimamo wa Urusi nchini Ukraine. Putin yuko sahihi kabisa!”

Uingiliaji kati wa sera za kigeni wa Kainerugaba haujawekwa tu kwenye mitandao ya kijamii.

Anasemekana kuwa alichangia pakubwa katika maelewano ya hivi majuzi kati ya Uganda na nchi jirani ya Rwanda na pia anadaiwa kuwa na jukumu muhimu katika operesheni ya pamoja iliyoanzishwa mwaka jana na vikosi vya Uganda na Congo dhidi ya kundi la waasi la Allied Democratic Forces mashariki mwa DR Congo.

Matarajio kuwa atapandishwa cheo na kuwa rais yamezusha hasira za wanasiasa wa upinzani na wakosoaji wa serikali, na kuwalazimu baadhi yao kwenda uhamishoni.

Mwandishi mashuhuri Kakwenza Rukirabashaija alikimbilia Ujerumani mwezi uliopita, kwa madai kwamba aliteswa rumande kwa tuhuma za kuwatusi Museveni na Kainerugaba.

Siku ya Jumanne, Kakwenza alikuwa miongoni mwa waliobashiri kuhusu mipango ya siku za usoni ya Kainerugaba, akitweet: "

“Pahali ambapo baba yake ataachia, mtoto wa kibaraka ataanzia hapo.”

“Tutaangamia ikiwa hatutazuia matarajio yake kuwa rais.”

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted