Afisa wa bunge: Watoto 71 wauawa nchini Ukraine kufikia sasa

Takriban watoto 71 wameuawa na zaidi ya 100 kujeruhiwa nchini Ukraine tangu Rais wa Urusi Vladimir Putin kuanzisha vita Februari 24, afisa wa bunge la Ukraine alisema Alhamisi.

0
Jengo la Hospitali ya watoto katika eneo la Kusini mashariki mwa mji wa Mariupol baada ya kushambuliwa mnamo Machi 9 2022. (Photo by Handout / National Police of Ukraine / AFP)

Takriban watoto 71 wameuawa na zaidi ya 100 kujeruhiwa nchini Ukraine tangu Rais wa Urusi Vladimir Putin kuanzisha vita Februari 24, afisa wa bunge la Ukraine alisema Alhamisi.

Idadi hiyo ilitangazwa huku kukiwa na ghadhabu juu ya shambulio la bomu Jumatano katika hospitali ya watoto huko Mariupol ambayo maafisa walisema iliua watu watatu, akiwemo msichana mdogo.

“Tangu mwanzo wa uvamizi wa Urusi hadi mwendo wa saa 11:00 asubuhi (0900 GMT) mnamo Machi 10, watoto 71 wameuawa na zaidi ya 100 wamejeruhiwa,” Lyudmyla Denisova, mjumbe wa bunge juu ya haki za binadamu, aliandika katika ujumbe wa Telegraph.

Hospitali hiyo ilipigwa wakati mji wa Mariupol, bandari ya kusini-mashariki mwa Ukraine, ikizingirwa na wanajeshi wa Urusi na watu wanaotaka kujitenga wanaounga mkono Urusi kutoka eneo la Donbas mashariki mwa Ukraine.

Vyanzo vya habari vilisema watu wazima 17 pia walijeruhiwa katika shambulio hilo la bomu.

Huko Malyn, katika eneo la Zhytomyr magharibi, watoto watatu na watu wengine wawili waliuawa wakati nyumba saba ziliharibiwa katika mashambulizi ya anga, kulingana na Denisova, ambaye alitoa mifano kadhaa ya watoto waliokufa katika mashambulizi ya anga.

Siku ya Jumatano usiku, wanawake wawili na watoto wawili waliuawa wakati kilipuzi kilipogonga nyumba yao huko Slobozhanske, kijiji kilichoko mashariki mwa mkoa wa Izium, Denisova alisema, akiongeza kuwa msichana wa miaka mitano alinusurika.

Huko Irpin, karibu na mji mkuu wa Kyiv, msichana mwenye umri wa miaka 10 alijeruhiwa vibaya na anapigania maisha yake hospitalini.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted