Matamshi huru au ya chuki? Hofu baada ya Elon Musk kuinunua Twitter

Wanaharakati wa kiraia wana wasiwasi kwamba Musk,atawaruhusu watu wenye msimamo mkali waliopigwa marufuku kurudi kwenye jukwaa hilo.

0
Elon Musk, mmiliki wa Tesla

Elon Musk anajielezea kama “mtu anayependa kuwepo kwa uhuru wa kusema,” na kuacha makundi ya haki za binadamu kuwa na hofu kwamba Twitter itakuwa jukwaa la matamshi ya chuki na habari potofu chini ya umiliki wake.

Tajiri huyo mkubwa zaidi duniani ameashiria kuwa, kufuatia ununuzi wake wa dola bilioni 44, ana nia ya kurekebisha kile anachokiona kuwa zuio la kujieleza kwenye Twitter.

Wanaharakati wa kiraia wana wasiwasi kwamba Musk, 50, atawaruhusu watu wenye msimamo mkali waliopigwa marufuku kurudi kwenye jukwaa hilo.

“Jambo ambalo hatuhitaji ni Twitter ambayo itafumbia macho kwa makusudi matamshi ya jeuri na matusi dhidi ya watumiaji, haswa wale wanaoathiriwa vibaya zaidi, wakiwemo wanawake, na makundi ya LGBTQ” Michael Kleinman, Mkurugenzi wa Teknolojia na haki za binadamu katika Amnesty International Marekani, alisema katika taarifa.

Kama mitandao mingine ya kijamii, Twitter imepambana dhidi ya taarifa potofu, uonevu na maudhui yanayochochewa na chuki katika miaka ya hivi karibuni.

Imepiga marufuku watumiaji wengi kwa kuendeleza vurugu au kutishia au kushambulia watu kwa misingi ya rangi zao, dini, utambulisho wa jinsia au ulemavu, miongoni mwa aina nyinginezo za ubaguzi.

Watu mashuhuri walioondolewa kwenye jukwaa hilo ni pamoja na kiongozi wa zamani wa Ku Klux Klan David Duke, mwanaharakati wa siasa kali za mrengo wa kulia Alex Jones, na rais wa zamani wa Amerika Donald Trump.

Twitter pia imedhibiti uongo kuhusu Covid-19 na kuondoa maelfu ya akaunti zilizohusishwa na vuguvugu la mrengo wa kulia la ‘QAnon’, ambalo wafuasi wake wanaamini kuwa Trump anapigana vita vya siri dhidi ya watu wanaoabudu shetani.

Wananadharia wengi walijiunga na majukwaa mapya zaidi kama vile Gab na Parler.

Trump, ambaye alipigwa marufuku baada ya kushambuliwa kwa Ikulu ya Marekani na wafuasi wake Januari 6 mwaka jana walipokuwa wakijaribu kutengua matokeo ya uchaguzi wa urais wa Marekani wa 2020, aliapa kutorejea Twitter hata kama Musk atamrejesha.

Lakini wahafidhina, ambao kwa muda mrefu wamelalamika kuhusu majukwaa ya mitandao ya kijamii yanayoendeshwa na waliberali wanaoishi Silicon Valley, wanatangaza mpango wa Libertarian Musk.

“Nina matumaini kwamba Elon Musk atasaidia kudhibiti historia ya Big Tech ya kudhibiti watumiaji ambao wana maoni tofauti,” Seneta wa Republican Marsha Blackburn alitweet.

Derrick Johnson, Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Kitaifa cha Maendeleo ya Watu Wa Rangi tofauti  (NAACP), alisema kuwa ingawa “mazungumzo huru yatakauwa bora, matamshi ya chuki hayakubaliki.’

‘Mjini Brussels, Shirikisho la Kimataifa la Waandishi wa Habari liliunga mkono wito huo, lilikuwa na wasiwasi kwamba bilionea huyo angeharibu uhuru wa vyombo vya habari “kwa kuzidisha fursa za kushambulia waandishi wa habari” kwenye tovuti.

Katibu Mkuu wa IFJ Anthony Bellanger alisema Twitter, ambayo ina watumiaji milioni 400, “lazima idhibitiwe ipasavyo, huku ikiheshimu uhuru wa kujieleza.”

Wataalamu wanasema kwamba mara tu atakaposhika usukani, Musk anaweza kugundua kwamba kuendeleza azma yake ya uhuru wa kujieleza sio rahisi sana.

Musk hajataja haswa ni vizuizi gani anakusudia kuweka, lakini alisema kwenye tweet Jumanne kwamba “anapinga udhibiti ambao unakiuka sheria.”

“Kama watu wanataka uhuru mchache wa kujieleza, wataiomba serikali kupitisha sheria kwa ajili hiyo. Kwa hiyo, kwenda nje ya sheria ni kinyume na matakwa ya watu,” aliongeza.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted