Nigeria: Wajumbe wa chama tawala wapiga kura kumchagua mgombeaji wa uchaguzi wa urais wa 2023

Zaidi ya wajumbe 2,300 wa APC walipiga kura kumchagua mgombea atakayekabiliana na Atiku Abubakar wa chama cha upinzani cha Peoples Democratic Party (PDP) katika kura ya urais ya...

0
Wajumbe kutoka sehemu mbalimbali za nchi wakusanyika katika mchujo wa chama tawala cha All Progressive Congress, Nigeria ili kumchagua mgombeaji wa urais wa chama hicho kwa ajili ya uchaguzi wa 2023 kwenye Ukumbi wa Eagle Square mjini Abuja, Nigeria Juni 8, 2022 (Photo by Kola Sulaimon / AFP)

Chama tawala nchini Nigeria cha All Progressives Congress (APC) kilipiga kura siku ya Jumatano katika chaguzi kuu za mchujo kumchagua mgombea katika uchaguzi wa mwaka ujao kuchukua nafasi ya Rais Muhammadu Buhari.

Hakuna mgombea anayependelewa zaidi kati ya viongozi wa APC wanaowania kuongoza nchi hiyo yenye watu wengi zaidi barani Afrika, akiwemo gavana wa zamani wa Lagos Bola Tinubu, Makamu wa Rais Yemi Osinbajo, waziri wa zamani wa uchukuzi Rotimi Amaechi na rais wa Seneti Ahmad Lawan.

Mkutano wa APC mjini Abuja ulifanyika siku mbili baada ya watu wenye silaha kuwaua watu 22 katika shambulio dhidi ya kanisa moja kusini magharibi — ukumbusho kwamba usalama katika uchaguzi utakuwa suala kuu.

Zaidi ya wajumbe 2,300 wa APC walipiga kura kumchagua mgombea atakayekabiliana na Atiku Abubakar, 75, wa chama cha upinzani cha Peoples Democratic Party (PDP) miongoni mwa wengine katika kura ya urais ya Februari 25.

Buhari, ambaye anastaafu baada ya mihula miwili anayoruhusiwa katika katiba, alifika katika kituo cha mikutano cha Eagles Square Jumanne jioni kabla ya upigaji kura kuanza mapema Jumatano.

Kiongozi huyo wa Nigeria alitumia siku kadhaa kabla ya mkutano mkuu wa chama katika mazungumzo na mirengo ya APC kutafuta umoja juu ya mgombea mmoja mwenye nguvu ingawa hakutoa dalili yoyote ya mgombea anayempendelea.

“Lazima tuchague mzalendo mwenye ujuzi, mwenye nia ya haki na mwenye imani kubwa sana katika umoja wa taifa letu, Nigeria, na nguvu ya tabia na madhumuni ya kuipeleka nchi mbele,” Buhari alisema katika hotuba yake kwenye mkutano huo.

“Hatupaswi kuruhusu PDP kurudisha nchi nyuma.”

Angalau wagombea watatu walijiondoa kwenye kinyang’anyiro hicho muda mfupi kabla ya upigaji kura kuanza, na wakawapa kura zao za ujumbe kwa Tinubu, gwiji wa APC na gavana wa zamani anayejulikana kama ‘Godfather of Lagos’.

Sehemu ya mjadala wa APC kuhusu wagombea inahusiana na ‘kugawa maeneo’– makubaliano yasiyo rasmi kati ya wasomi wa kisiasa kwamba urais wa Nigeria unapaswa kuchukua nafasi kati ya wale kutoka kusini yenye Wakristo wengi na wale kutoka kaskazini eneo lenye Waislamu wengi.

Baada ya mihula miwili na Buhari muislamu wa kaskazini, waangalizi walitarajia urais kwenda kwa mgombea kutoka kusini.

Lakini PDP — ambayo ilifanya mchujo wake Mei 28 na 29 — ilimchagua Abubakar, makamu wa rais wa zamani na nguli wa kisiasa ambaye ni Muislamu wa kaskazini.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted