Mabwenyenye Tayari Kutoa Mkwanja Kuinunua Manchester United.

Ractliffe mwenye umri wa miaka 70 na kampuni yake tayari wamewasilisha ofa ya kutaka kununua asilimia 69 ya kuinunua Man United.

0

Bwenyenye na shabiki sugu wa Manchester United Jim Ractliffe sasa anasema kuwa “huwa hafanyi tu maamuzi bila kuzingatia matokeo yake “,hii ikionyesha kuwa uwezekano wa mwanabiashara huyo kununua kilabu ya Manchester United ni mkubwa mno.


Ractliffe mwenye umri wa miaka 70 na kampuni yake tayari wamewasilisha ofa ya kutaka kununua asilimia 69 ya kuinunua Man United.


Ratcliffe anamiliki timu ya kuendasha baiskeli ya INEOS Grenadiers,kilabu ya Nice inayoshiriki ligi ya soka Ufaransa,kilabu ya FC FC Lausanne-Sport inayopiga katika ligi ya uswizi na robo ya timu ya Mercedes inayoshiriki mashindano ya mbio za magari ya langalanga Formula 1.


Hata hivyo Ratcliffe anapata ushindani mkubwa kutoka kwa wanunuzi wengine ambao wameonyesha nia ya kuinunua man United wakiwemo Sheikh Jassim Bin Hamad Al Thani na Hamad Bin Jassim Bin Jaber Al Thani ni mwanawe waziri mkuu wa zamani wa Qatar.Ofa yake Hamad Bin Jassim Bin Jaber Al Thani ni ya kumiliki kilabu ya man United kwa asilimia 100.


Sheikh Hamad bin Jassim bin Jaber Al Thani amekuwa ikihudhuria mechi ya Manchester United katika uwanja wa Old Trafford na mechi za ugenini.


Sheikh Hamad bin Jassim bin Jaber Al Thani amewasilisha ofa ambayo haihusiani na kampuni ya Qatar Sports Investments (QSI) wala mamlaka ya kuekeza ya Qatar (QIA).


Ofa ya Qatar kwao Manchester United inadaiwa kuwa na uwezo wa kumaliza madeni yote ambayo united inadaiwa ikiwa pauni milioni £515.


Familia ya Glazer inapania kuuza asilimia 50 ama zaidi yake kwa wawakezaji.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted