‘Mbakaji wa Facebook’ Thabo Bester, aliyekamatwa Tanzania arejeshwa Afrika Kusini

Thabo Bester, aliyepatikana na hatia ya ubakaji na mauaji, alitoroka kutoka gereza la kibinafsi huko Bloemfontein Mei mwaka jana

0

Tanzania imemfukuza mmoja wa wakimbizi waliokuwa wakitafutwa zaidi nchini Afrika Kusini, mbakaji na muuaji Thabo Bester, ambaye alidanganya kifo chake akiwa gerezani na kisha kukimbilia katika taifa hilo la Afrika Mashariki.

Thabo Bester, aliyepatikana na hatia ya ubakaji na mauaji, alitoroka kutoka gereza la kibinafsi huko Bloemfontein Mei mwaka jana, lakini polisi wa Afrika Kusini waligundua mwezi uliopita.

Mpenzi wake, daktari maarufu Nandipha Magudumana, ambaye alikamatwa naye, pia amefukuzwa nchini.

Babake Zolile Sekeleni, ameshtakiwa kwa kumsaidia Bester kutoroka gerezani. Sekeleni na mlinzi wa gereza aliyesimamishwa kazi, Senohe Matsoara, wameshtakiwa kwa mauaji, kuchoma moto na kusaidia kutoroka kwa Bester.

Bester aliaminika kufariki baada ya kujichoma moto akiwa jela, lakini mwishoni mwa mwezi Machi polisi walisema uchunguzi wa DNA ulibaini kuwa mabaki yaliyokuwa yameungua yaliyopatikana kwenye seli yake yalikuwa ya mtu mwingine.

Aliyepewa jina la “mbakaji wa Facebook”, Bester, ambaye alihukumiwa kifungo cha maisha jela kwa ubakaji, wizi na mauaji mwaka wa 2012, aliwarubuni waathiriwa kwenye mtandao huo wa kijamii kabla ya kuwabaka na kuwaibia. Aliua angalau mwathirika mmoja.

Siku ya Jumamosi, Waziri wa Sheria wa Afrika Kusini Ronald Lamola alitangaza kuwa Bester alikamatwa na mamlaka ya Tanzania Ijumaa usiku pamoja na mwanamke, raia wa Msumbiji.

Siku ya Alhamisi, Lamola alisema wawili hao wamerejeshwa Afrika Kusini.

“Tunaweza kuthibitisha kwamba wakimbizi hawa wamerudishwa Afrika Kusini” kutoka Tanzania, Lamola aliuambia mkutano na waandishi wa habari mjini Cape Town.

“Bw Thabo Bester amerejeshwa tena katika kituo kikuu cha marekebisho cha Kgosi Mampuru”, Lamola alisema, akiishukuru serikali ya Tanzania.

Mwanamke huyo alikuwa amekamatwa akisubiri kufikishwa mahakamani baadaye siku ya Alhamisi, alisema.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted