Watu 11 wahukumiwa kifo nchini Tanzania kwa mauaji ya mhifadhi

Mahakama nchini Tanzania iliwahukumu kifo watu 11 siku ya Ijumaa kutokana na mauaji ya mhifadhi maarufu Wayne Lotter mwaka wa 2017

0

Mahakama nchini Tanzania iliwahukumu kifo watu 11 siku ya Ijumaa kutokana na mauaji ya mhifadhi maarufu Wayne Lotter mwaka wa 2017.

Lotter, mwenye umri wa miaka 51 kutoka Afrika Kusini anayeishi Tanzania, alikuwa mwanzilishi wa PAMS Foundation ambayo ilifanya kazi kukomesha ujangili wa tembo na usafirishaji wa pembe za ndovu nchini Tanzania.

Aliuawa kwa kupigwa risasi jijini Dar es Salaam akiwa ndani ya teksi akirejea kutoka uwanja wa ndege.

Sababu kamili ya mauaji yake bado haijajulikana lakini wenzake wa Lotter wanaamini alilengwa kwa kazi yake ya kulinda tembo.

“Baadhi ya washukiwa hao katika taarifa zao zilizorekodiwa na askari polisi, walikiri kushiriki katika mikutano ya kula njama na kuua,” hakimu Laila Mgonya aliiambia mahakama. “Ushahidi uliotolewa ulikuwa na nguvu za kutosha kuwatia hatiani.”

Utoaji wa hukumu za kifo si jambo la kawaida nchini Tanzania lakini kwa ujumla wao hubadilishiwa maisha jela.

Unyongaji wa mwisho kutekelezwa nchini ulikuwa mnamo 1994.

Tanzania imekuwa miongoni mwa nchi za Kiafrika zilizokumbwa na uwindaji haramu wa tembo, ikipoteza zaidi ya tembo 66,000 katika kipindi cha muongo mmoja, lakini jitihada za kuwazuia watu hao zinamaanisha kuwa ujangili umepungua katika miaka ya hivi karibuni.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted