Raila Odinga Astaafu Kama Mwakilishi Mkuu Wa Umoja Wa Afrika Kwa Maendeleo Ya Miundombinu

Taarifa ya kustaafu kwake Odinga ilitangazwa na mwenyekiti wa tume ya Umoja wa Afrika Moussa Faki Mahamat.

0

Hatimaye muda wa kuhudumu wa aliyekuwa waziri mkuu nchini Kenya Raila Odinga kama mwakilishi mkuu wa umoja wa Afrika katika miundommbinu na maendeleo umefikia tamati.


Taarifa ya kustaafu kwake Odinga ilitangazwa na mwenyekiti wa tume ya Umoja wa Afrika Moussa Faki Mahamat.


Umoja wa Afrika kupitia Faki umempongeza Odinga kwa kuwa nguzo kuu ya uboreshaji wa miundomsingi wakati wa hatamu yake.


“Tunakupongeza zaidi kwa jukumu lako,umekuwa wa thamani zaidi.Tunaomba kukushukuru zaidi kwa kukubali mwito wa kuwahudumu katika wadhifa uliotwikwa wakati wa kipindi cha mpito,” alisema Faki.


Umoja wa Bara Afrika (AU) umepokeza majukumu haya sasa kwa shirika la NEPAD ambalo litaendesha idara hiyo.


Raila Odinga hata hivyo ameushukuru Umoja wa Afrika kwa nafasi aliyopewa kuhudumu. Katika barua rasmi kwa AU, Odinga amedokeza kuwa katika makala ya pili ya mkutano wa miundommbinu na maendeleo wa Umoja wa Afrika, aliangaazia baadhi ya changamoto anazokumbana nazo kuwajibikia majukumu yake kikamilifu.


“Nashukuru zaidi hatua za haraka ambazo umoja wa Afrika umechukua ili kuniruhusu kushughlikia masuala mengine ya kidharura”alisema odinga kupitia Barua.


Odinga aliteuliwa katika wadhifa huo Oktoba 20, 2018 wakati wa utawala wa aliyekuwa rais wa nne wa jamhuri ya Kenya Uhuru Kenyatta.


Kiongozi huyo alikuwa na afisi mbili, moja jijini Nairobi Kenya na nyingine jijini Addis Ababa Ethiopia ambapo makao makuu ya AU yapo.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted