Aliyekuwa Kocha Wa Harambee Stars Adel Amrouche Ateuliwa Kocha Wa Taifa Stars Ya Tanzania

Amrouche,58, amewai kuitia makali timu ya soka ya Burundi, Equatorial Guinea, Botswana, Libya na Yemen

0

Aliyekuwa kocha mkuu wa timu ya soka ya Kenya Harambee Stars Adel Amrouche, ameteuliwa mkufunzi mkuu wa timu ya Tanzania, Taifa Stars.

Menaja mkuu wa mawasialiano katika shirikiso la mpira wa kabumbu TFF Bwana Clifford Mario, amesema Amrouche amekuwa na rekodi nzuri ikiwemo kutwaa ubingwa wa CECAFA akiwa mkufunzi wa Harambee stars na kuweka rekodi ya kutofungwa mechi 20 kwa mpigo.

Amrouche mwenye umri wa miaka 58 raia wa ubelgiji na uasilia ya Algeria, amewai kuitia makali timu ya soka ya Burundi, Equatorial Guinea, Botswana, Libya na Yemen.

Kwenye taarifa ya awali, Kocha Wa Yanga Bwana Mohamed Nasridane alikuwa ni mmoja wapo wa alikuwa amepigiwa upato kuchukuwa wadhiwa huwo lakini shirikisho la Mpira wa mguu ya Tanzania TFF ikabadili maneno na kumpa Amrouche Kandarasi hiyo.

Kocha huyo alipigwa kalamu Na FKF baada ya misururu mbaya ya matokeo kwa timu ya Harambee stars mwaka wa 2014 hususan katika mechi za kufuzu kwa kombe la mabingwa barani Africa, AFCON

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted