Mtu mmoja hufariki kwa ajali kila wiki jijini Mwanza nchini Tanzania 

Upande wa pikipiki zimetokea ajali kubwa 30 kwa kipindi hicho cha Januari hadi Desemba, 2022 zilizosababisha vifo vya watu 25 na kujeruhi watu 26

0

Ikiwa leo ni maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama nchini Tanzania imeelezwa kuwa kwa mwaka 2022 ajali kubwa 81 zilitokea mkoani Mwanza na kusababisha vifo 71 na majeruhi 96.

Kwa mujibu wa Mkuu wa mkoa huo, Adam Malima amesema kutokana na takwimu hizo wastani wa mtu mmoja na zaidi hufariki dunia kutokana na ajali kila wiki.

“Ndugu zangu hiki ni kiwango cha juu sana kwamba kwa kila wiki moja inatokea ajali kubwa ambayo inaondoa binadamu mmoja Mwanza, kwa wastani binadamu mmoja na zaidi,” amesema Malima

Amesema kwa upande wa pikipiki zimetokea ajali kubwa 30 kwa kipindi hicho cha Januari hadi Desemba, 2022 zilizosababisha vifo vya watu 25 na kujeruhi watu 26.

“Mwelekeo wa takwimu hizi sio mzuri kabisa na hivyo nina wataka watumiaji wote wa barabara katika Mkoa wa Mwanza kuzingatia kanuni na sheria za usalama barabarani ili kuweza kupunguza idadi hii ya majeruhi na vifo vya wananchi wenzetu.
“Chanzo kikubwa cha ajali za barabarani ni makosa ya kibinadamu, moja ni madereva kutokufuata sheria za usalama barabarani, nyingine ni mwendo kasi uliopitiliza ambao mara nyingi hauna sababu wala malengo ya huko anapoelekea.
“Nyingine ni madereva kuendesha magari wakiwa wamelewa au kuendesha kwa saa zilizopitiliza mfululizo mpaka usingizi unamchukua,” amesema Malima.
Amesema wapanda pikipiki nao hawavai kofia ngumu na kupakia abiria zaidi ya mmoja, maarufu kwa jina la mishikaki.
“Kwa hiyo ni imani yangu kwamba kwa elimu itakayotolewa katika kipindi hiki cha maadhimisho itakuwa ni chachu kwa madereva, wapanda pikipiki na makundi yote ya watumiaji barabara Mkoa wa Mwanza na maeneo mengine,” amesema. Wakati leo ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama nchini Tanzania imeelezwa kuwa kwa mwaka 2022 ajali kubwa 81 zilitokea jijini Mwanza na kusababisha vifo 71 na majeruhi 96.

Mkuu wa mkoa huo, Adam Malima amesema kutokana na takwimu hizo wastani wa mtu mmoja na zaidi hufariki dunia kutokana na ajali kila wiki.

“Ndugu zangu hiki ni kiwango cha juu sana kwamba kwa kila wiki moja inatokea ajali kubwa ambayo inaondoa binadamu mmoja Mwanza, kwa wastani binadamu mmoja na zaidi,” amesema Malima

Amesema kwa upande wa pikipiki zimetokea ajali kubwa 30 kwa kipindi hicho cha Januari hadi Desemba, 2022 zilizosababisha vifo vya watu 25 na kujeruhi watu 26.

“Mwelekeo wa takwimu hizi sio mzuri kabisa na hivyo nina wataka watumiaji wote wa barabara katika Mkoa wa Mwanza kuzingatia kanuni na sheria za usalama barabarani ili kuweza kupunguza idadi hii ya majeruhi na vifo vya wananchi wenzetu.

Kwa mujibu wa mkuu huyo wa mkoa ni kwamba chanzo kikubwa cha ajali za barabarani ni makosa ya kibinadamu, moja ni madereva kutokufuata sheria za usalama barabarani, nyingine ni mwendo kasi uliopitiliza ambao mara nyingi hauna sababu wala malengo ya huko anapoelekea.

“Nyingine ni madereva kuendesha magari wakiwa wamelewa au kuendesha kwa saa zilizopitiliza mfululizo mpaka usingizi unamchukua,” amesema Malima.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted