Kenya: Naibu Rais William Ruto ndiye mgombea urais anayependwa zaidi, kulingana na matokeo ya kura ya maoni

Utafiti huo pia ulifichua kuwa wengi wa wafuasi wa Naibu Rais  Ruto ni vijana wenye umri wa miaka 18-35, huku Odinga akiungwa mkono na wazee.

0
William Ruto, Naibu Rais Kenya

Kura ya maoni mpya iliyofanywa na shirika la utafiti la Trends and Insights For Africa (TIFA) inaonyesha kuwa chama cha Naibu Rais William Ruto cha United Democratic Alliance (UDA) ndicho chama maarufu zaidi kwa asilimia 34.

Kikifuatwa na Orange Democratic Movement (ODM) cha Raila Odinga kwa asilimia 19, Jubilee kwa asilimia 4 na Wiper kwa  asilimia 3.

Matokeo ambayo pia yalimweka Ruto mbele yalitolewa na Mchambuzi wa Utafiti wa TIFA Tom Wolf.

Wolf alieleza kuwa ODM ya Odinga na UDA ya Ruto ndivyo vyama pekee vinameweza kupata kuungwa mkono kote nchini kulingana na makadirio yao.

Kuhusu mgombea urais aliyependekezwa zaidi nchini Kenya Naibu Rais William Ruto alidumisha uongozi kwa asilimia 39, akifuatiwa kwa karibu na Raila Odinga.

Wolf alibainisha kuwa idadi kubwa ya Wakenya bado hawajaamua kuhusu mgombea urais wanayempendelea kwa asilimia 16, huku asilimia 12 wengine wakiwa hawana nia ya kujibu swali hilo.

Utafiti huo pia ulifichua kuwa wengi wa wafuasi wa Naibu Rais  Ruto ni vijana wa Kenya wenye umri wa miaka 18-35, huku Odinga akiungwa mkono na Wakenya wazee.

Utafiti huo ambao ulifanywa katika mikoa 9 pia ulionyesha kuwa Odinga bado ni maarufu Nyanza, Mashariki na Nairobi, huku Ruto akiwa maarufu katika Bonde la Ufa ikifuatiwa na Mlima Kenya.

Utafiti huo ulifanyika kati ya Aprili 22 na 26, na ulifanywa kupitia mahojiano ya simu katika lugha zote mbili za Kiswahili na Kiingereza.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted