Rais Samia aunda Kikosi Kazi cha kushughulikia Nishati Safi ya Kupikia

Rais Samia Suluhu ameshiriki katika Kongamano la Nishati safi iliyoandaliwa na Wizara ya Nishati chini ya Waziri January Makamba.

0

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu ameshiriki katika Kongamano la Nishati safi iliyoandaliwa na Wizara ya Nishati chini ya Waziri January Makamba.

Kongamano hilo limefanyika jijini Dar es salaam huku likihudhuriwa na watu mashuuri. Prof. Anna Tibaijuka, ambaye ni Waziri Mstaafu akabainisha moja ya chanzo ambayo inawafanya wananchi wengi kutumia kuni na mkaa, kama chanzo cha nishati ya kupikia ni kupanda kwa gharama za kujaza mitungi ya gesi, kitolea mfano kujaza gesi zamani ilikuwa ni Tsh 18,000 kwa mtungi mdogo, sasa ni Tsh 24,000.

 Amesema tatizo ndo lilipoanzia hapo. Waziri wa nishati January Makamba amesema kupika chakula si adhabu hadi upike huku unatoa kamasi na machozi.

Rais wa Tanzania Samia Suluhu amesema watu wengi wanatumia nishati ya kuni na mkaa kwa ajili ya kupikia ambazo zinaleta changamoto ya kiafya na mazingira, amesema kaya zinazopikia gesi ni 5%, umeme ni 3% huku vyanzo vingine safi ni 2.2%.

Rais Samia amebainisha kuwa tatizo la maji linalalamikiwa sana na wakaazi wa Dar es salaam linachangiwa na ukataji miti kwa wingi mkoani Pwani, ambako kuna mto Ruvu unaosambaza maji jiji Dar, hivyo amewasihi wananchi kuacha kukata miti badala yake watumie nishati nyingine bora zaidi.

Rais Samia ametoa maelekezo ya kuundwa kwa Kikosi kazi ambacho kitashughulikia nishati safi ya kupikia na ameshauri kisiwe cha Serikali pekee, bali kihusishe sekta binafsi na watu wengine.

Kikosi kazi hiki kitaongozwa na Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa na kuratibiwa na Wizara ya Nishati .

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted